Hivi karibuni kulizuka mapigano makali wilayani Mvomero
kati ya wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai na yalisababisha mkulima mmoja
kupoteza maisha.
Morogoro:KATIKA kile kinachoonekana
kuwa ni ubunifu wa hali ya juu, mfugaji mmoja, Msimbe Jonas wilayani Mvomero amebuni mbinu mpya ya kuzuia mbuzi wake kuingia katika mashamba ya
wakulima na kula mazao yao.
Mwandishi wetu aliyekuwa
Mvomero vijijini hivi karibuni alishuhudia Jonas akiwa na mbuzi wake
ambao amewatengenezea chombo (plastiki) na kuwafunga midomo yao ili kuwazuia
kula mazao katika mashamba ya watu.
“Nimebuni mbinu hii ya
kuwazuia mbuzi wangu kula mashamba kwa kuwafunika midomo. Huwa naenda nao hivi
hadi mbali kabisa na mashamba ya watu, huko nawafungua ili wale majani,
wameshazoea,” alisema Jonas.
Aliongeza kwamba mbinu hiyo
ni nzuri na imemfanya asiwe na wasiwasi anapopitisha mbuzi wake karibu na
mashamba ya wakulima.“Baadhi ya wakulima walioona mbuzi wangu wakiwa hivi
wamefurahia sana ubunifu wangu huu,” alisema Jonas.
Mbuzi wakiwa wamezibwa midomo
Hivi karibuni kulizuka mapigano makali wilayani Mvomero
kati ya wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai na yalisababisha mkulima mmoja
kupoteza maisha.
Wakulima nao wakaamua kulipiza kisasi kwa kuchoma moto nyumba za Wamasai zaidi ya 50 na kusababisha hasara kubwa kwa jamii hiyo.