Treka Cristian Ronaldo sasa yu fiti kwaajili ya kulisakata
kabumbu na kuisaidia timu yake Real Madrid kuweza kujinyakulia ushindi. Kauli
hiyo imethibitika baada ya kuchezea timu yake hiyo na kuweza kupata ushindi wa
goli 1-0 dhidi ya Bayern Munich.
Supastaa huyo wa kireno alipoteza muelekeo wake tangu siku
timu yake ya Real Madrid ilipocheza na Dortmund kwenye kombe la UEFA mnamo
tarehe 2 mwezi April. Katika mchezo huwo Real Madrid iliweza kujichukulia
ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya wapinzani wao. Katika mchezo huwo ndipo mchezaji
huyo nyota Ronaldo alipoumia goti.
Hapa amenukuliwa akisema “Najisikia fiti na nipo tayari kwa
mchezo unaofuata” akaongeza tena na kusema “Kwasasa najiamini sana kwasababu
najisikia safi kabisa. Sina maumivu yoyote na kwa hivyo namaanisha nipo fiti”