Mapigano makali yanaendlea baina ya wafugaji wa kimasai na wakulma eneo la Matui huku chanzo cha mapigano hayo kikisemekana kuwa ni kugombeamaeneo ya kufanyia shughuli za kilimo na ufugaji.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa wananchi wa eneo hilo wameyakimbia makazi yao wakihofia kupoteza maisha yao. Hivyo wananchi hao wamekusanyika kwenye kituo kidogo cha Polisi kwaajili ya usalama wao.
Chanzo cha habari hii kimeendelea kutaarifu kuwa kundi kubwa la Wamasai kutoka sehemu mbalimbali nchini kama vile Mererani na Simanjiro wamedhamiria kwenda kuwasaidia wenzao kwenye mapigano hayo.