
Alisema alichukua chepe na kumpiga nalo mara mbili sehemu ya
kichwani hadi alipoanguka na kuzirai. Alisema baada ya hapo, alitoa ripoti
polisi ambao walifika na kumchukua.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete jana aliwatunuku nishati
Watanzania 28, akiwamo muuza chips, Kassim Said Kassim (28), ambaye aliyepewa
nishani na ushupavu baada ya kupambana na kumdhibiti jambazi mwenye silaha.
Hafla ya utoaji wa nishani hizo ilifanyika jana jioni katika Viwanja vya
Ikulu na kuhudhuriwa na mabalozi na viongozi mbalimbali wa Serikali, huku
Kassim akiwa kivutio kutokana na idadi kubwa ya watu kushangazwa na ujasiri
wake wa kupambana na jambazi mwenye silaha.
Kijana huyo alikuwa wa mwisho kutajwa na baada ya mshereheshaji wa hafla
hiyo kueleza historia yake kwa kifupi kwamba alizaliwa mwaka 1986, iliibuka
miguno kutoka kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo na aliposimulia kisa
chenyewe, kila mtu aliduwaa. Baadaye Kassim alimweleza mwandishi wetu:
“Nilikuwa nafanya biashara ya chips eneo la Buguruni Malapa. Nakumbuka Julai 7, mwaka jana saa tatu usiku tulivamiwa na jambazi aliyekuwa na bastola na kuanza kuwatishia wateja, akitaka kupatiwa fedha na vitu mbalimbali.
“Nilikuwa nafanya biashara ya chips eneo la Buguruni Malapa. Nakumbuka Julai 7, mwaka jana saa tatu usiku tulivamiwa na jambazi aliyekuwa na bastola na kuanza kuwatishia wateja, akitaka kupatiwa fedha na vitu mbalimbali.
“Kwanza alianza kuwashinikiza wateja wampatie fedha na alipoona hakuna
aliyemsikiliza, alichomoa bastola na kumtishia mmoja wa wateja, hapo ndipo
nilipoamua kupambana naye.”
Alisema alichukua chepe na kumpiga nalo mara mbili sehemu ya kichwani hadi
alipoanguka na kuzirai. Endelea>>