Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015
saa 9:30 Alasiri.
1.0 Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa
mujibu wa aya ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka
1997. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama Na. 4/2011, Tume ya
Utumishi wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri
watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.
1.1 Hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia
watanzania wenye sifa zilizo ainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na
ambao wapo tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania ambazo zipo
katika mikoa na wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
2.0 Afisa utumishi II (TGS D) - Nafasi 80.
2.1 Sifa:
Shahada
ya kwanza ya sayansi ya jamii au sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyo
tambulika na serikali ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani
zifuatazo:-
- Menejimenti ya rasilimali watu (Human resource management)
- Elimu ya jamii (Sociology)
- Utawala na Uongozi (Public Administration)
- Mipango ya watumishi (Manpower planning)
- Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
2.2 Waombajin watapangiwa kazi Mahakama za wilaya isipokuwa
za mkoa wa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe wilaya tatu (3)
zilizopo katika mojawapo ya mikoa ifuatayo: Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara,
Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na
Shinyanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza
lisizingatiwe. Aidha, baadaye watabadilishwa kazi kuwa watendaji wa Mahakama.
2.3 Kazi za Afisa utumishi Daraja la II
(i) Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote.
(ii) Kutafsiri na kushughulikia miundo ya utumishi.
(iii) Kutafiti, kuchanganua, kupanga, na kukadiria idadi ya
watumishi wanao hitaji mafunzo.
(iv) Kukusanya, kuchambua, na kupanga takwimu na kumbukumbu
zote zinazohusu mipango ya watumishi.
(v) Kushughulikia masuala mbalimbali ya kila siku ya
watumishi.
(vi) Kusimamia OPRAS
3.0 Afisa Tawala II - TGS D - Nafasi 80
3.1 Sifa
Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyo tambuliwa na
serikali katika fani zifuatazo:-
Utawala, Elimu ya jamii, Sheria (Mwenye cheti cha Law
school), Menejimenti ya Umma, Uchumi na wenye ujuzi wa kompyuta.
3.2 Waombaji watapangiwa kazi katika mahakama za Wilaya
isipokuwa za mkoa wa Dar es Salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe wilaya
tatu (3) zilizopo katika mojawapo ya mikoa ifuatayo:- Pwani, Morogoro, Lindi,
Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu,
Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro,
Tanga na Shinyanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza
lisizingatiwe. Aidha, baadaye watabadilishwa kazi kuwa Watendaji wa Mahakama.
1.3 Kazi za Maafisa Tawala
(i) Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu.
(ii) Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na
taratibu mbalimbali.
(iii) Kusimamia kazi za Utawala na Utendaji.
4.0 Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani (Internal Auditor) Daraja la
II TGS D - Nafasi 25
4.1 Sifa
(i) Wenye Intermediate Certificate inayo tolewa na NBAA.
(ii) Wenye shahada ya Biashara au Sanaa yenye mwelekeo wa
uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu (UDA) kutoka Chuo au Taasisi yoyote
inayo tambuliwa na Serikali.
(iii) Wenye Stashahada ya juu katika Uhasibu wa Serikali
(Advanced diploma in Government Accounting) kutoka chuo cha uhasibu Dar es
salaam (DSA)
4.2 Waombaji watapangiwa kazi Mahakama Kuu - Kanda au Ofisi
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi isipokuwa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii
waonyeshe Kanda/Mikoa mitatu (3) kati ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara,
Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na
Shinyanga ambayo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao laweza
lisizingatiwe.
4.3 Kazi za Mkaguzi wa Hesabu za Ndani Daraja la II
(i) Kufanya ukaguzi wa Hesabu.
(ii) Kusahihisha na kuidhinisha ripoti ya Ukaguzi.
(iii) Kusahihisha na kuidhinisha hoja za ukaguzi wa ndani (
Internal Audit queries)
5.0 Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D -
Nafasi 15.
5.1 Sifa
Shahada/Stashahada ya Juu katika masomo ya Sayansi ya
Kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinacho tambuliwa na Serikali.
5.2 Waombaji watapangiwa kazi Mahakama Kuu - Kanda isipokuwa
Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe kanda tatu (3) kati ya
zifuatazo: Arusha, Bukoba, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mwanza, Mtwara,
Songea, Sumbawanga, Tabora na Tanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa
pendekezo lao linaweza lisizingatiwe.
5.3 Kazi za Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja II
(i) Kuweka kumbukumbu za taratibu za kisasa na mbinu za
kufanyia kazi.
(ii) Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za
taarifa na udhibiti unaohusu Kompyuta.
(iii) Kutoa msaada wa kiufundi kwa Wizara/Idara/Vituo
mbalimbali vya kazi.
6.0 Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015
saa 9:30 Alasiri.
7.0 Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na
kuambatanisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV)
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Waombaji walio katika utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha
maombi yao kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa Umma
waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa Umma.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi
wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P 8391, DAR ES SALAAM.
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.
CHANZO: HABARI LEO 2nd February 2015.