
Wasichana wanaojihusisha na biashara ya kujiuza wakiwa sokoni
Msako huo unatokana na malalamiko ya muda mrefu ya wakazi
wa Jiji la Tanga hususan wanaoishi mitaa ya Centrol na Ngamiani ambako biashara
hiyo inadaiwa kukithiri.
Tanga. Polisi mkoani hapa wamesema wataendesha msako wa
kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ngono katika nyumba za starehe na mitaa
maarufu kwa biashara hiyo.
Msako huo unatokana na malalamiko ya muda mrefu ya wakazi
wa Jiji la Tanga hususan wanaoishi mitaa ya Centrol na Ngamiani ambako biashara
hiyo inadaiwa kukithiri.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, Freisser Kashai alisema wamepokea malalamiko hayo muda
mrefu, walishindwa kuchukua hatua mara moja kwa kuwa walikuwa wakiyafanyia
uchunguzi. Alisema baada ya kumalizika kwa uchunguzi wao, wamejipanga
kuwakamata wote wanaohusika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Kamanda huyo alisema kuendelea kuiacha ishamiri inachangia kuporomosha maadili
ndani ya jamii.
Kamanda Kashai alisema cha kusikitisha, biashara hiyo
sasa inafanywa mpaka na watoto wadogo wenye umri wa kwenda shule na wanafunzi
wanaosoma shule za bweni ambao wengi hutoroka nyakati za usiku na kwenda
kujiuza kwenye nyumba za starehe.
Alisema polisi wana taarifa zote za majengo na maeneo
kunakofanyika biashara hiyo. “Operesheni yetu itaanza muda wowote kuanzia sasa,
tutawakamata na kuwafikisha mahakamani,” alisema.
Akizungumzia usalama wa raia na mali zao katika sikukuu
ya Mwaka Mpya, Kamanda Kashai ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa
kwa polisi pale watakapobaini viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.
“Kila mara tumekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na
wananchi mitaani kuwaelimisha namna ya kushirikiana na Polisi kuwafichua
wahalifu, hii imesaidia kupunguza matukio hayo kwa asilimia kubwa,” alisema
Kashai.
Ctrdt: Mwananchi