Mwili wa Kijana baada ya kuchomwa kisu
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamisi Selemani (18)
mkazi wa Vingunguti jijini Dar es salaa, amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu
maeneo ya kifuani kwake.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa Hamis
ameingia katika mauti hayo baada ya kufumaniwa na msichana anayedaiwa kuwa ni
mpenzi wa mtu (Jina limehifadhiwa) mwenye miaka 15. Mtu ambaye anatuhumiwa kutenda tukio hilo
amefahamika kwa majina ya Ali Kimondo ambaye ndiye anayedaiwa kuwa mpenzi wa msichana huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia
mwaka mpya majira ya saa 9:00 usiku katika eneo la Vingunguti Magenge.
Nzuki aliendelea kueleza kuwa baada ya tukio hilo Ali
Kimondo pamoja na msichana huyo walitoroka, kwa namna hiyo Jeshi la polisi
linaendelea na upelelezi kwaajili ya kuwapata watuhumiwa hao.