
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu
akiutubia mkutano wa hazara mjini Nansio Wilaya ya Ukerewe,
Mwanza lengo kushukulu wananchi kwa kukipatia ushindi katika uchaguzi wa
Serikali za mitaa uliopita. Wilaya hiyo Chadema imepata
viti 47 vya Serikali za vijiji huku ccm ikipata 27 na CUF viwili.
Picha na Jovither Kaijage
Akizungumzia hatua hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nansio
jana, Mwalimu ambaye ameanza ziara mkoani hapa juzi kwa lengo la kuwashukuru
wananchi baada ya kukichagua chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,
alisema hakuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na viongozi hao.
Ukerewe. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amemsimamisha
kazi mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho Wilaya ya Ukerewe, Wilbrod
Machemli kwa kushindwa kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kutotangaza
ujio wa kiongozi huyo.
Rungu hilo pia limemkuta katibu wa Chadema wilaya hiyo, Libelatus Mlebele
ambaye amepewa onyo kali.
Akizungumzia hatua hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nansio
jana, Mwalimu ambaye ameanza ziara mkoani hapa juzi kwa lengo la kuwashukuru
wananchi baada ya kukichagua chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,
alisema hakuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na viongozi hao.
Kutokana na hali hiyo, Mwalimu alimwagiza Mwenyekiti wa wilaya wa chama
hicho, Jacobo Munyaga kwa gharama zake amwandalie mkutano mwingine kabla ya
mwisho wa mwezi ujao.
Mwalimu pia alitilia shaka matumizi ya fedha yaliyotajwa kutumika kutangaza
uwepo wa mkutano wake.
Alisema Chadema hakipo tayari kulinda viongozi wazembe na wasiowajibika na
kuwaonya wajumbe wa kamati tendaji hasa katibu ambaye bado yupo katika
uangalizi wa miezi sita kwa maelezo kuwa anaweza kuondolewa kazini.
Kabla ya kuchukua uamuzi huo, Mwalimu aliwaita mbele wakazi wanne wa kata za
Kakerege, Nansio, Nakatungulu na Kagera ambao walikiri kutosikia matangazo ya
ujio wake.
Hatua hiyo aliichukua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Mongera wa mjini
Nansio saa 9:30 alasiri huku kukiwa na idadi ndogo ya watu ikilinganishwa na
ziara zake za nyuma.
Mbali na hilo, pia Mwalimu ametumia mkutano huo kukemea matumizi mabaya ya
fedha za serikali yanayofanywa na viongozi waandamizi wakati huduma za kijamii
zikizidi kuwa mbaya.
Alisema ziara za mara kwa mara za nje ya nchi zisizo za lazima zinazofanywa
na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine hazina tija kwa taifa.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi akizungumza
katika mkutano huo, alisema katika katika kipindi cha miaka minne ya uongozi
wao wamepata mafanikio makubwa.
Alisema mbali na kusimamia vyema matumizi ya fedha za serikali katika
utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pia halmashauri hiyo imekamilisha mipango
ya kununua greda moja la kutengeneza barabara lenye thamani ya Sh400 milioni
hivi karibuni chama hiko kimeluwa kikipigania kukishinikiza serikali
kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.
Hata hivyo, alisema mbali ya halmashauri hiyo kupata hati
safi ya matumizi ya fedha za umma pia hivi karibuni huko jijini Nairobi Kenya,
Halmashauri hiyo ilipata tuzo ya kukidhi vigezo vya sheria ya ununuzi ya umma
kati ya wilaya 166 za nchi nzima.
Crdt: Mwananchi