Mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edward Ngoyai Lowassa amewataka wananchi kisiwani Pemba kumkataa na kuto mchagua mgombea yeyote anaye chezea amani ya nchi  kwani nchii hii similiki ya mtu bali nimali ya watanzania wote na kusisitiza kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anapambana na umasikini kwa nyanja zote.

Mh.Lowassa alie wasili kisiwani Pemba na kusindikizwa na vijana kwa Pikipiki Vespa na Magari hadi hapa kiwanja cha  kibirinzi ambapo mkutano wa kampeni ulifanyika na kuwataka wananchi wa Pemba  kumkataa mgombea anae tishia  amani na utulivu kwani ndio itakayo weza kusaidia kufikisha malengo ya kuleta mageuzi ya kweli katika nyanja zote za maendeleo na kuahidi  kuwa ataimarisha Hospitali kila wilaya kwakuweka vifaa vya kisasa.

Mh .LowasSa amesesisitiza kuwa endapo atakuwa rais wa Tanzania atahakikisha anabadilisha mitaala ya elimu kuwa ya kisasa ilikuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania.



Mapema mgombea mwenza wa rais wa jamhuri ya  mungano  wa Tanzania kupitia umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Juma Duni Haji  amewataka wazanzibar kushirikiana ilikufanya mabadiliko kwa amani na utulivu nae mgombea urais wa Zanzibar  kupitia chama cha wananchi CUF Malim Seif Sharifu hamadi ameendelea kussisitiza kuwa chama chake cha  wananchi CUF hakina  mpango wa kufanya vurugu kama inavyo daiwa.
Chanzo: ITV

 
Top