Waziri wa haki nchini Misri Ahmed al-Zind amefutwa kazi baada yake kujigamba kwamba angeweza kumfunga jela hata Nabii Muhammad mwenyewe iwapo angevunja sheria.

BwZind alisema hayo kwenye mahojiano katika runinga Ijumaa.
Baada ya kugundua kosa lake, mara moja alisema “Mungu nisamehe”.
Siku iliyofuata pia aliomba radhi.

Amefutwa kazi na Waziri Mkuu Sherif Ismail

Haijabainika bara moja ni nani atachukua nafasi ya Bw Zind, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa kundi la Muslim Brotherhood.

"Waziri Mkuu Sherif Ismail ametoa agizo leo la kumuondolea Ahmed al-Zind ... wadhifa na majukumu yake," taarifa ilisema.

Majaji wa Misri baadaye wametoa taarifa wakishutumu hatua ya kumfuta kazi Bw Zind.

Mkuu wa chama cha majaji hao Abdallah Fath ameambia Reuters kwamba ni ulimi tu uliteleza hilo linaweza kumtendekea mtu yeyote.

Mtangulizi wa Bw Zind alifutwa kazi baada ya kusema mwana wa mzoaji taka hawezi kuhudumu kama jaji.

Chanzo: BBC

 
Top