Nabii kairuki ambaye kabla ya Kumpokea Yesu kristo aliwahiu kuwa mwanachama wa Freemason, Amekanusha madai ya kwamba msanii mshuhuri wan bongo flavor  (Diamond) kuwa aliwahi kuwa mwanachama wa chama hicho cha Freemason.

Kwakuthibitisha hayo Nabii Kairuki amezungumza na gazeti la Visa na kusema kuwa mtu yoyote akiwa mwanachama wa chama hicho anakuwa na alama, na hata kama akiacha alama hiyo haifutiki inaendelea kuwepo. Diamond hana alama hiyo kwa mujibu wa Nabii huyo.

Kitu pekee ambacho anakitumia Diamond katika mafanikio yake ni majini ya kichawi ambayo yapo saba. Nabii Kairuki anaendelea kusema kuwa kuna utofauti kati ya Freemason na uchawi. Kwamujibu wa kimtazamo vitu hivi viwili vinawiana kwasababu vyote vinamtumikia shetani. Utofauti wake ni kwamba Uchawi unajiendesha kibinafsi wakati Freemason inajiendesha kichama na taasisi.


Kwa mujibu wa maelezo ya nabii Kairuki anadai kuwa anampenda sana Diamond hivyo anamshauri awachane na majini hayo kisha amrudie Mungu. Na endapo hatofanya hivyo mwisho wa msanii huyo unaweza kuwa wa majuto.


PICHA HII NI DIAMOND AKIWA NA TUZO YAKE
 
Top