Mtu mmoja wilayani Serengeti mkoani Mara katika kijiji
cha Nyatwari, amenusurika kupoteza maisha kutokana na kichapo kikali
alichokipokea kutoka kwa wananchi.
Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika kutokana
na mazingira ya tukio lenyewe, aliingia katika kichapo hicho baada ya kunywa
pombe na kuanzisha vurugu.
Mtu huyo ambaye alikuwa akifahamika kuwa alikuwa ni
Mgambo aliamua kutumia cheo cha upolisi kufanya vurugu hizo jambo ambalo
halikuwafurahisha baadhi ya watu na kuamua kujichukulia sharia mkononi hadi
alipokuja kuokolewa na askari wa jeshi la polisi.