Mahabusu wa Gereza la Biharamulo mkoani Kagera wamefanya
mgomo baada ya kusota kwa miaka mitatu ndani pasipo kusikilizwa mashauri yao.
Ameeleza mtoa habari wetu kuwa Mahabusu wa Gereza hilo wanaotuhumiwa
kuwa na kesi za mauaji wameamua kuchukua jukumu hilo wakiamini kuwa ni njia
itakayoweza kuwashinikiza mahakama Kusikiliza kesi zao ambazo nyingine ni za
zaidi ya miaka mitatu.
Baada ya kupata Habari hiyo Utamu war aha ilifanya
jitihada za kumtafuta mkuuwa gereza hilo ili kuzungumzia suala hilo lakini
haikufanikiwa kwa simu yake kutokupatikana.