Hebu fikiria uko labda umekaa na mtoto anacheza vizuri tuu mara gafla kaanguka pah! chini, na hapumui ama mapigo ya moyo yamesimama, ukiangalia vizuri, mtoto anaanza kubadilika rangi. Ama unapigiwa simu na house girl, mama mtoto ameacha kupumua gafla, Je jambo la kwanza utachofanya itakuwa nini? Well, majanga hutokea its a matter of being prepared with the right skills, ready.


Just the other day, nilikuwa naangalia news, nikaona anti mmoja alivyokuwa amechanganyikiwa pale ambapo karibia apoteze maisha ya kichanga/kitoto chake. The moment was scary lakini niliona ni jinsi gani situation ya huyo dada ilivyokuwa surreal kwamba ingeweza kumtokea mtu/mama/dada yeyote?

Long story short, anti huyo alikuwa ndani ya gari na mtoto mchanga aliyekuwa nalia sana. Well, nnje kulikuwa na joto kali mno na magari yalikuwa katika foleni isiyo sogea. Fumba fumbua, mtoto alikuwa ameacha kulia bila sababu. Yole anti akashuka ndani ya gari mbio mbio na kwenda nyuma ili kumwangalia mtoto hali yake. Fumba fumbua, mtoto ameacha kupumua na ameanza kubadilika rangi. Anti kwa akili ya chap chap akamtoa mtoto kwenye car seat(kiti chake) na kuanza kumwita jina huku akimnyanyua juu (amepanic) ili apatiwe msaada na mtu yoyote. Anti huyu anasema hata vidole vilishindwa kufanya kazi ya kupiga 911 ili waje kumsaidia.

Bahati nzuri msamaria mwema akatokea, kizuri zaidi alikuwa anajua kutoa huduma ya kwanza, basi ndo akaanza kumshughulikia mtoto chap chap huku na yeye akiwa haelewi afanye nini kingine.
Epic moment: mtoto alianza kupumua na dispatch wakawa ndo wamefika na kumchukua mtoto mbio mbio hospitali.
 


Well, lesson learned. sasa tujifunze nini. Well, unless wewe ni nesi(nurse) ama docta na unajua cha kufanya in such situation, pale mtu anapo undergo cardiac arrest (mapigo ya moyo yana simama na mtu anaacha kupumua), well, inabidi ujifunze jinsi ya kutoa first aid. Ni performance ndogo lakini inaweza/inaokoa maisha ya mtu. In this case maisha ya mtoto.

Okay, so cha msingi nini?
Kwanza kabisa piga 911 kama uko nchi za nje. Kama bongo of course, mayowe kwa nguvu lakini kumbuka kufanya hivi vituatavyo pia: first aid/huduma ya kwanza/basic life support/CPR ni ilee-ile moja kwa mtoto na mtu mzima kinachobadilika tuu ni jinsi inavyotolewa.
 

MAMA: mtoto mtoto amelala chini hapumui.
Jibu: mwite mtoto kwa nguvu (jina lake), mguse mguse uone kama atasogea. angalia kifua chake kama kina panda na kushuka (kuashiria mtoto ana mapigo ya moyo)

MAMA: mtoto anamapigo ya moyo lakini hapumui
Jibu: mnyanyue kichwa kidogo ili kufungua njia ya hewa. mfunge mtoto pua na vidole vyako viwili na mpumulie pumzi mtoto pumzi puf ya kwanza msikilize kama ameanza kupumua. kama hapumui mpulizie tena pumzi ya pili. endelea kumsikiliza kama anapumua, na endelea na process ya kumpulizia pumzi hivyo hivyo na kumsikiliza mpka msaada uje.
 
msikilize mtoto kama anapumua kwanza na kama ana mapigo ya moyo

CHA KUZINGATIA: mtoto hapumui, mtoto hana mapigo ya moyo
Jibu: baada ya kumpumulia mtoto, weka vidole vyako viwili chini na katikati ya chuchu za mtoto, halafu sukuma kifua chake taratibu ila haraka haraka kidogo ukihesabu mara 30. msikilize mtoto kama anapumua kwa kuweka shavu lako karibu na pua na mdogo wa mtoto. kama mtoto hapumui, mpulizie pumzi na mdogo wako huku ukiwa umemziba pua, then angalia kama kifua chake kina panda na kushuka, kama hana mapigo ya moyo, msukume tena na vidole vyako viwili katikati ya kifua chake mara 30. huku ukisubiri msaada uje wedha ni 911 ama majirani.

KAMA NI MTU MZIMA: utafanya hivi hivi pia ila kumbuka kuchukua tahadhari na kutumia kitambaa kabla ya kumpumulia mtu ama kumsukuma kifua chake na viganja vya mikono yako.


PICHA KWA MIFANO ZAIDI
 
Mpinde kicwa kidogo ili kufungua njia ya hewa


 
Njia ya hewa ikiwa imefunga (Picha ya juu)
Njia ya hewa ikiwa imefunguaka (Picha ya chini)

 
mzibe mtoto pua na vidole viwili halafu mpumulie pumzi, moja then msikilize kama ana pumua, then pumzi ya pili.

 

kama mtoto hapumui na hana mapigo ya moyo. ukisha mpumulia pumzi, weka vidole vyako viwili kama inavyoonyesha kwenye picha na sukuma kifua chake huku ukishindilia kidogo mara thelathini (sukuma, moja, sukuma, mbili na kuendelea mpaka 30)
 
 
kumbuka kuchukua tahadhari kwanza

  
 
kama ni mtu mzima/kijana/msichana, msukume kwenye kifua na viganja kama waliovyoonyesha kwenye picha mara thelathini. halafu sikiliza pumzi na mapigo ya moyo, then kama hakuna, endelea kufanya hivyo mpaka msaada uje

SOURCE: tzmomz.com


 
Top