Katika
kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na
Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama
hukupata kusikiliza wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya
uwasilishwaji wa Ripoti hiyo.
“…Katika
fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya
viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi
wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.
Kwa upande
wa Viongozi wa Kisiasa walioingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni;
Mheshimiwa Andrew Chenge Mbunge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi Bil.
1.6,mheshimiwa Anna Tibaijuka Mbunge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, shilingi Bil. 1.6, Mheshimiwa William Ngeleja Mbunge na ambaye alikuwa
Waziri wa Nishati na Madini, shilingi milioni 40.4, ndugu Daniel Yona ambaye
alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4, ndugu Paul
Kimiti, ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4
na ndugu Enos Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCo aliingiziwa
shilingi milioni 161.7…“– Zitto Kabwe.
“… Kamati
imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja
na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea
Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.
Kwa upande
wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo
kwenye ripoti ya CAG kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu
alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota fedha kwenye
akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati za ofisi ya CAG
ulionyesha kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati
imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia muamala
huu usifanyike…“– Deo Filikunjombe.
Kamati kwa
kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri Mkuu
alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala huu
usifanyike, ndio maana katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu
alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo
Filikunjombe.