Mbu anaye eneza ugonjwa wa Dengue 'Aedes egyptiae'
Ugonjwa uliojizolea umaarufu kwa
ghafla na kupatiwa majina lukuki kama vile Dengu, Denguo, Denge, Dengue, nk.
Unaendelea kutikisa jiji la Dar salaam na baadhi ya mikoa ya jirani kwa
kuwakamata watu wengi zaidi na kusababisha vifo kwa wagonjwa. Watu wamepoteza
amani na kujawa na hofu kubwa juu ya gonjwa hilo.
Wakati amani ikitoweka kwa upande
mwengine juu ya gonjwa hilo wananchi walio wengi wa hali ya chini wamepoteza
imani zaidi ya kuishi kutokana na gharama ambayo inatumika kufanyiwaa uchunguzi
wa maambukizi ya ugonjwa huwo.
“Yani wakati ugonjwa wa Dengu
unatunyanyasa wananchi, kwa baadhi ya wenzetu wanauchukulia ugonjwa huu kama
mtaji” alisema James Anord mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
“Yaani nimekwenda kupimwa
hospitali ya Kairuki baada ya kuhisi hali yangu haipo vizuri. Lakini baada ya
kupimwa vipimo vyote sikukutwa na tatizo lolote. Daktari alinishauri nipime
Denguo na Gharama za vipimo hivyo ni shilingi Elfu Arobaini (40,000/=).
Nilishituka sana baada ya kusikia kiasi hicho cha pesa. Daktari aliniambia kuwa
gharama hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na vituo vingine vya afya” alisema
Anita Mwanafunzi wa shule ya Uandishi wa habari (SJMC).
Gharama za upimaji wa ugonjwa huu
wa dengue katika vituo mbalimbali vya afya ambavyo ni binafsi ni ghali kiasi
cha kufikia shilingi 50,000/= hadi 80,000/= kwa upande wa vituo vya afya vya
serikali gharama zake ni kati ya shilingi 25,000/= na 30,000/=.
Gharama za upimaji zipo juu zaidi
kuliko gharama za matibabu, kwani endapo ukibainika kuwa umepata maambukizi ya
ugonjwa huwo gharama za matibabu ni kati ya shilingi 200/= na 500/=