Wakati watu wakifikiri tatizo la mauaji ya ndugu zetu wenye
ulemavu wa ngozi kufutika, jana mkoani Simiyu kumetokea tukio la kushitusha
ambapo mwanamke mmoja anayeitwa Mughu Lugata (40) anayeishi katika kijiji cha
Gasuma wilayani Bariadi ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga kisha baadhi ya
viungo vyake kutoweka na wahalifu wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa kamanda wa mkoa Charles Mkumbo amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo kijiji hapo, ambapo marehemu alivamiwa na watu hao akiwa
nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana. Wahalifu hao walitoweka na baadhi ya
viungo vya marehemu kama vile mguu wa kushoto, vidole viwili vya mkono wa
kushoto, pamoja na ukucha wa kidole gumba.
Inasemekana chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina
walizonazo baadhi ya watu kuwa Viungo cha Albino ni chanzo cha utajiri.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa uhalifu huwo
likisaidiana na wananchi.