Njiwa
Njiwa aliyekuwa na hirizi alizua taflani na kashehe baada ya kuingia kwenye wodi  namba tatu Mwaisela katika hospitali ya Muhimbili. Wagonjwa waliokuwemo katika wodi hiyo walijikuta wakipoteza amani na matumaini ya kupona baada ya kumuona ndege huyo akizunguuka wodini.

Njiwa huyo zunguuka wodini humo na kwenda kutua kwenye dirisha moja lililokuwepo karibu na kitanda cha mgonjwa. Ndugu wa mgonjwa alijaribu kumkamata njiwa huyo na wakati huwo huwo mtu mwengine mwenye mgonjwa kitanda cha jirani alipandisha mashetani na kusema kuwa dege huyo alikuwa amekwenda hospitalini hapo kwaajili ya kummaliza mgonjwa aliyekuwepo kwenye kitanda kilichokuwepo karibu na dirisha.


Njiwa huyo baada ya kukamatwa alikabidhiwa katika kampuni ya ulinzi ya NGE. Na kutokana na watu kuwa wengi wakishangaa tukio hilo, walinzi walipata jukumu la kuwaondosha raia hao.
 
Top