TABIA HATARISHI NI ZIPI?

Mtu anayetumia dawa za kulevya hasa yule anayejidunga yupo katika hatari ya kuambukizwa VVU. Hata hivyo wale ambao huwa katika maeneo yenye utumiaji wa dawa za kulevya wana hatari zaidi ya kuambukizwa VVU kwa kufanya ngono zisizo/salama na watumiaji wa dawa hizo.

Aidha, vijana wenye umri wa kupevuka wapo katika hatari zaidi ya kuambukizwa zaidi kwenye tabia hatarishi kuliko makundi mengine.

Zipo tabia nyingi ambazo humweka mtumiaji wa dawa za kulevya katika hatari kubwa ya kuambukizwa VVU. Zifuatavyo ni baadhi tu ya tabia hizo:
  • Kutumia mara kwa mara na kwa muda mrefu dawa za kulevya.
  • Kushirikiana dawa, sindao, au mabomba na vifaa vingine vya kujidunga.
  • Kusafisha vifaa vya kujidunga walivyoshirikiana bila kufuata taratibu zinazoweza kuua vijidudu,
  • Kufanya ngono ziizo salama.
  • Kuwa na wapenzi wengi (Kubadilisha wapenzi) kununua penzi kwa dawa au fedha.
  • Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
  MAMBO GANI HUCHOCHEA TABIA HATARISHI?
Uelewa mdogo juu ya tabia zenyewe hatarishi
  • Mtazamo potofu kuwa kushirikiana sindano au mabomba ni ishara ya uaminifu na undugu miongoni mwa wanaojidunga.
  • Misukumo rika.
  • Arosto kali inayotokana na utegemezi 
  • kuzoeleka kwa matumizi ya dawa za kulevya kaka jamii zetu.
  • Ugumu wa maisha.
HUDUMA GANI ZICHUKULIWE KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU?
Kiongozi:
  • Kuweka sera zisizo kandamiza, zisizo bagua na zisizo watega watu wanaotumia dawa za kulevya ili waweze kuzitumia huduma za tiba.
  • Kuelimisha umma juu ya tabia za dawa za kulevya na maambukizi ya VVU.
  • Kuhaikisha programu za kuwasaidia  watumiaji wa dawa za kulevya zinaanzishwa na kuendelezwa.
Mwananchi:
  •  Kuto wanyanyapaa na kuto wabagua watumiaji wa dawa za kulevya na badala yake kuwachukulia kuwa watumiaji ni watu wanaohitaji msaada wa matibabu na kuwaelekeza sehemu watakapozipata huduma za tiba.
Mtumiaji wa dawa za kulevya:
  • Kuacha kutumia zadawa za kulevya
  • Kuacha kushirikiana indano au mabomba na vifaa vingine vinavyotumika kujidunga 
  • Kusafisha vyema vifaa vya kujidunga kwa kuchemsha au kutuia dawa za kusafishia.
Somo hili limetayarishwa na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Kitalu Naba 434, Barabara ya Malik, Upanga, SLP 80327, Dar es alaam, Tanzania.



________________________________________________________________________________


  • Magonjwa Ya ngono na Vijana
 Soma hapa>>

________________________________________________________________________________
  • Sababu Zinazopelekea Vijana Kupia mande/Mtungo Read More>>
___________________________________________________________________
 
Top