Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikiria mkazi mmoja mkoani Tabora walayani Igunga kijiji cha Itumba kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu na nyara za serikali.
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Bwana Bundala aliyekuwa akitokea mkoani Tabora kuja mkoani Singida kuwasalimia ndugu zake ambao walikuwa wamewekwa maabusu katika kituo cha Polisi cha wilaya ya Ikungi.
Kamanda Sedoyeka amesema mbinu waliyo tumia kumkamata mtuhumiwa huyo ni baada ya askari kumtilia mashaka na kuamua kumkagua wakati akisubiri kuwasalimia ndugu zake ambao ni maabusu na kukuta vipande viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya chatu, vipande vya ngozi ya simba, pembe ambayo haija julikana na chupa tatu za mafuta ya simba.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida wameliomba jeshi la Polisi kuhakikisha, linamfuatilia mtuhumiwa huyo ili kuweza kubaini mtandao mzima kwa sababu za imani potofu ikiwemo kupata madaraka wana sababisha vifoo vya binadamu ikiwemo wenye ulemavu wa ngonzi Albino.

 Chanzo ITV
 
Top