Pichani ni Mke wa Marehemu Kambi

Mwishoni mwa wiki iliyopita dereva wa bodaboda aliyetajwa kwa jina moja la Kambi (33), anadaiwa kuchinjwa na kufa papohapo.


Tukio hilo lilitokea juzikati majira ya saa 11:00 alfajiri ambapo mwili wa bodaboda huyo uliokotwa maeneo ya Modeko jirani na Makutano ya Barabara za lringa na Mazimbu na kusababisha mkewe kuchanganyikiwa huku ndugu wakiwa hawaamini.


Marehemu Kambi Enzi za Uhai wake

Muda mfupi baada ya tukio hilo, Chanzo chetu cha habari kilifika eneo la tukio na kuushuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umetupwa lakini hawakuchukua chochote kutoka kwa marehemu huku wakimwachia bodaboda yake na waleti ikiwa na fedha taslimu shilingi laki 240,000.


Ngugu na jamaa wa marehemu Kambi wakiwa katika shughuli za Msiba


Kufuatia hali hiyo baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, walidai huenda jamaa huyo alifumaniwa na mke wa mtu kwani mara ya mwisho alionekana akiwa amempakiza mwanamke hivyo kuna madai kwamba mwenye mali hakuwa na sababu ya kuchukua chochote zaidi ya kumtoa roho.

Majira ya saa 12:00 asubuhi, polisi walifika eneo hilo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka mochwari kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho kilifika eneo la tukio kilidai kuwa, jamaa huyo aliuawa katika tukio lililohusisha fumanizi la mke wa mtu kwani baada ishu hiyo wahusika walitoka nduki bila kuchukua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
 
Top