Mwanamke mmoja mkoani Tabora (Jina limehifadhiwa) mwenyeji wa mtaa wa Kazaroho Kata ya Mbuyuni amenusurika kufa baada ya mume wake kumkata sehemu zake za siri.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kilifika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoani Tabora na kupana nafasi ya kuzungumza na mwanamke aliyefanyiwa unyama huo na mume wake.
Mwanamke huyo alieleza kuwa, Siku ya tukio mume wake; 'Mashaka' alifika nyumbani kwake mchana kutokea kwenye mihangaiko yake akiwa ameongozana na mtu mwingine ambaye alidaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji.
Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina moja tu la Mashaka alimueleza kuwa mtu aliyekuwa ameongozana naye alikuwa ni mganga wa kienyeji na alikuwa akitafuta sehemu za siri za mwanamke, hivyo alimsihi mke wake akubali kutoa viungo vyake kwani ni dili kubwa na wangeondokana na umasikini. Hata hivyo mwanamke huyo amedai kuwa alikataa na kumfanya Mashaka kuondoka na mganga wake.
"Usiku nilipokuwa nimelala mume wangu alinikata na kuniamuru nisipige kelele kwakuwa alikuwa amekwishapatana bei na ulikuwa ni utajiri mkubwa" alizungumza kwa taabu mwanamke huyo
Alieleza kuwa baada ya tukio hilo alijikuta amelazwa Hospitalini hapo na haelewi kama mume wake Mashaka amekwisha kamatwa au laa.
Kwa mujibu wa majirani zake mtaa wa Kazaroho walisema kuwa lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana, na wasamalia wema ndio waliomsaidia kumfikisha Hospitalini hapo.
Mwanamke aliyekatwa sehemu zake za siri na mume wake aliyefahamika kwa jina moja la Mashaka.
BOFYA HAPA KUPATA MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA