Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa mtoto mmoja mdogo
mvulana wa miaka miwili amempiga risasi kimakosa mama yake mzazi na kumuua
ndani ya duka moja kubwa la uuzaji bidhaa la Wal-Mart.
Maafisa wa usalama wanasema bunduki iliyotumika iliyokuwa imefichwa ilichomoka wakati mvulana huyo alipokaribia na kuligusa begi la mkononi la mama yake mwenye umri wa miaka 29.
Maafisa wa usalama wanasema bunduki iliyotumika iliyokuwa imefichwa ilichomoka wakati mvulana huyo alipokaribia na kuligusa begi la mkononi la mama yake mwenye umri wa miaka 29.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Hayden, katika jimbo
la Idaho.
Msemaji wa Kaunti hiyo anasema mwanamke huyo alikuwa na
kibali cha kumiliki silaha.
Chanzo: BBC