
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisser Kashai
Mama wa marehemu, Abida Zuberi alisema jana kuwa tukio hilo
lilitokea juzi usiku. Alisema siku hiyo mtoto huyo alikwenda kulala kwenye
nyumba ya dada yake ambaye amelazwa hospitali.
Handeni.
Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kivesa wilayani Handeni
Mkoa wa Tanga, Isiyaka Beda (14) amefariki dunia baada ya kunyongwa na kuvunjwa
shingo na watu wanaodaiwa kuwa ni wezi.
Mama
wa marehemu, Abida Zuberi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku.
Alisema siku hiyo mtoto huyo alikwenda kulala kwenye nyumba ya dada yake ambaye
amelazwa hospitali.
Zuberi
alisema mwanaye aliombwa na shemeji yake akalale huko kwa kuwa yeye amesafiri
kikazi.
Alisema
usiku wakati Beda amelala waliingia watu katika nyumba hiyo yenye vyumba viwili
na sebule na kwenda chumbani alimolala kisha wakamnyonga na kuiba magodoro na
runinga na wakatokomea.
Alisema
asubuhi yake alipigiwa simu na mkwe wake (mume wa mtoto wake) kuwa amerudi
safari ila hali aliyoikuta kwake siyo nzuri.
“Aliniambiwa
kuna wezi wamevunja milango na kuiba, lakini nikamuuliza Beda mzima...Hakutoa
jibu la moja kwa moja ndiyo nikaamua kurudi nyumbani nikamkuta amefariki
dunia,” alisema.
“Wezi
hao walivunja chumba cha kwanza na baadaye kuingia alikolala Beda. Mimi nipo
hospitali kwa wiki nzima sasa ninamuuguza mwanangu mwingine,” alisema.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisser Kashai alisema uchunguzi wa kifo hicho bado
unaendelea ili kuwabaini waliohusika.
Aliwataka
wananchi kutoa taarifa polisi kwa kuwataja watu wanaodhani kuwa ndiyo wahusika
wakuu kwenye masuala ya uhalifu katika jamii ili sheria ichukue mkondo wake.
Crdt: Mwananchi