Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola
Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya
Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba
na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.
Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel,
mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada
ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa
majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe
wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.
Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza
Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina
matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake
akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa
na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.
Chanzo: BBC
KWA HABARI ZAIDI ZA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>