KUDINDA MAANA YAKE NI NINI?
Kipindi cha balehe mvulana huanza kudindisha (uume kusimama) Hali hii hutokea wakati ambapo chembechembe za ndani ya uume hujaa damu zaidi ya kawaida.


Chembechembe hizo zilizopo ndani ya uume zinapojaa damu huwa ngumu na kusababisha uume kuongezeka unene na urefu na kuwa mgumu (husimama).

Kudinda kwa uume kunaweza kutokea ama kwa haraka sana au taratibu. vilevile uume huweza kudinda kwa muda mfupi au mrefu. Hali hii ni ya kawaida kwa wavulana na wanaume wote.

KWANINI UUME HUDINDA?
Kudinda kunaweza kutokea kwa mvulana ama mwanaume wakati wa kuamka asubuhi, au anapokuwa na wasiwasi, uume unapoguswa au mvulana ama mwanaume anapofikiria masuala ya ngono.

Wakati mwingine hali hii ya kudinda huweza kutokea bila ya sababu yoyote. Hali hii ni ya kawaida hasa katika kipindi cha kubalehe.

Kudindisha wakati mwingine huweza kutokea wakati mtu hategemei jambo ambalo linaweza kumfanya mvulana kuhisi aibu, lakini ni hali ya kawaida sana kwa wavulana na hali hii huwa inapungu kadri anavyokuwa.

JINSI YA KUHIMILI HALI YA KUDINDISHA.
kijana wa kiume huweza kudindisha wakati wowote na mahali popote, kwamfano inaweza kutokea kijana yupo darasani, ama hata akiwa amekaa pembeni mwa barabara.

Mara nyingi hali hii hutokea pasipo kutegemea. ni hali ya kawaida lakini huweza kumfanya kijana wa kiume hasa wale wanaoanza kubalehe kuhisi aibu.

Baadhi ya mapendekezo ya kuhimili kudindisha ni pamoja na kubaki umekaa kama ulikuwa umekaa, Kuvaa suruali pana, kuweka mikono kwenye ifuko ya suruali hasa kama utakuwa unatembea, Funika kwa kitu kama vile kitabu ama begi kwa wanafunzi, Kuwaza mambo mengne mpaka hali hiyo iishe ama ipotee
          Fungua masomo ya Vijana hapa>>                                                   


 
Top