Alianza kwa ibada kabla ya kuingia kwenye mto wenye kina kirefu na kuanza kutembea akiwa na malengo ya kufanya kama alivyofanya Yesu.

Tukio hili la kustaajabisha limetoke huko nchini Nigeria ambapo Mchungaji mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Kabele, amezama kwenye mto huku waumini wake wakishuhudia.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa, Mchungaji Mabele alianza na kuwaambia waumini wake kuwa ili kupita juu ya maji ni lazima kuwa na imani ya kutosha. Hivyo aliwaahidi kufanya kitendo hicho ili kuwathibitishia waumini wa dini hiyo uzito wa imani yake.

Matebele alianza na kufanya maombi na baada ya maombi alitumbukia kwenye mto huo mkubwa wenye kina kirefu. Mambo yakawa tofauti na vile waumini pamoja na yeye mwenyewe alivyotarajia, kwani alizama na kuinua mikono kuomba msaada.

Haikuwa rahisi kwa waumini hao kutoa msaada kwa kiongozi wao wa dini kutokana na ukubwa wa mto wenyewe. Hivyo mchungaji Matebele alipoteza maisha huku waumini wake wakishuhudia na wasijue cha kufanya.
 Mikono ya Mchungaji Matebele akijaribu kuomba msaada kwa waumini wake

KUPATA MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>  
 
Top