Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale anapenda kuwatangazia watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi zifuatazo;

NAFASI; MLINZI (NAFASI 1)

SIFA
• Awe amehitimu kidato cha nne na kufuzu mafunzo ya Mgambo/Polisi/JKT au mafunzo ya Zimamoto kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali
• Awe na umri wa kuanzia miaka 18-44.

KAZI ZA KUFANYA
• Kuhakikisha mali yoyote ya Ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idgini
• Kuhakikisha mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake
• Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku
• Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi
• Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la Ofisi wanaidhini ya kufanya hivyo
• Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
Mshahara
• Mshahara kwa nafasi hiyo ni TGS 'A' sawa naTshs.265,OOO/= kwa mwezi.

Utaratibu wa uombaji

Maombi yote yaletwe yakiwa na nakala halisi za vyeti vya Elimu na Taaluma pamoja na wasifu wa mwombaji (CV)
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S. L. P. 23, LIWALE.
Mwisho wa kutuma maombi ni tar 21 Novemba, 2014 saa 9.30 alasiri.
_____________________________________________________________________________


NAFASI; MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (NAFASI 2)
 
Sifa
• Kuajiriwa wahitimu wa kidalo cha nne wenye cheti cha Utunzaji wa Kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.
• Awe na umri wa kuanzia miaka 18-44.

Kazi za kufanya
• Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka/Mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
• Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu Inyaraka.
• Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika(Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
• Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File racks/cabinales katika masjala/vyumba pa kuhifadhia kumbukumbu.
• Kuweka kumbukumbu (barua, nyarakan.k) katika mafaili
• Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutokaTaasisi za Serikali.
Mshahara
• Mshahara kwa nafasi hiyo ni TGS 'B' sawa naTshs.345,OOO/= kwa mwezi.

Utaratibu wa uombaji
Maombi yote yaletwe yakiwa na nakala halisi za vyeti vya Elimu na Taaluma pamoja na wasifu wa mwombaji (CV)
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S. L. P. 23, LIWALE.
Mwisho wa kutuma maombi ni tar 21 Novemba, 2014 saa 9.30 alasiri.

_____________________________________________________________________________
 
NAFASI; KATIBU MAHSUSI III (NAFASI 3)
 
Sifa
• Awe amehilimu kidalo eha nne na kuhudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Halua ya tatu.
• Awe amefaulu somo la HatiMkaloya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya
• Kompyuta kutoka chuo chochole kinachotambuliwa na Serikali na kupata Cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Intemet.E-Maii na Publisher.

Kazi za kufanya
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifalkumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo Ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyasawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinanohusika.
• Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wakazi.
Mshahara
• Mshahara kwa nafasi hiyo ni TGS 'B' sawa na Tshs.345,OOOI= kwa mwezi.

Utaratibu wa uombaji

Maombi yote yaletwe yakiwa na nakala halisi za vyeti vya Elimu na Taaluma pamoja na wasifu wa mwombaji (CV)
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S. L. P. 23, LIWALE.
Mwisho wa kutuma maombi ni tar 21 Novemba, 2014 saa 9.30 alasiri.

_____________________________________________________________________________NAFASI; 

MTENDAJI WA KIJIJI III (NAFASI 8)
 
Sifa
• Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha nne (IV) au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
• Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:-
• Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za
Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa n'a Serikali.
Kazi za kufanya
• Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na malizao.
• Kuratibu na kusimamia upangaji na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
• Kutafsiri na kusimamia sera, sheria naTaratibu.
• Kuandaa Taarifaza Utekelezajiwa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza uzalishaji mali.
• Kiongozi wa Wakuu waVitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
• Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
• Kusimamia Utungajiwa Sheria ndogo za Kijiji.
• Atawajibika kwa Mtendajiwa Kata.
Mshahara
• Mshahara kwa nafasi hiyo ni TGS 'B' sawa naTshs.345,OOOI= kwa mwezi.

Utaratibu wa uombaji

Maombi yote yaletwe yakiwa na nakala halisi za vyeti vya Elimu na Taaluma pamoja na wasifu wa mwombaji (CV)
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S. L. P. 23, LIWALE.
Mwisho wa kutuma maombi ni tar 21 Novemba, 2014 saa 9.30 alasiri.

 FUNGUA NAFASI ZAIDI ZA AJIRA BOFYA HAPA>> 
 
Top