Kaling Wald mwenye umri wa miaka 50 alipatikana na makosa ya kushindwa
kuwaarifu maafisa wa polisi kwamba mumewe alifariki ,kosa ambalo na akahukumiwa
kuwekwa katika muda wa majaribio na ushauri,wakili wake alikiambia chombo cha
habari cha Reuter siku ya Jumanne.
Peter Wald mwenye umri wa miaka 52 alifariki mnamo mwezi machi mwaka 2013
kwa kile mamlaka inasema ni sababu za kawaida kufuatia maambukizi ya mguu wake
yanayodaiwa kusababishwa na ugonjwa wa sukari.
Mkewe Kaling Wald alimwacha kitandani na kufunga chumba hicho katika nyumba
yao ya Hamilton ,Ontario ili kuzuia harufu kali iliokuwa ikitoka chumbani humo
kuwafikia watu waliokuwa wakiishi nyumbani humo.
Kama vile Yesu alivyomfufua Lazaro baada ya siku ya nne ,pia yeye aliamini
kwamba Mungu atamfufua mumewe wakili wa mwanamke huyo alisema.
Source BBC