Nieto ,nahodha wa kilabu ya kijimbo ya Tiro federal alishambuliwa na genge
baada ya mechi kati ya wapinzani wao wa jadi Chacarita Juniors katika mji wa
Aimogasta kazkazini magharibi mwa Argentina.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa dakika 15 kabla ya kukamilika baada ya refa
kuwapa kadi nyekundu wachezaji wanane kwa kupigana.
Mwaka huu watu 15 wamefariki katika ghasia zilizosababishwa na soka nchini
Argentina,Binamu wa Nieto,Pablo Nieto amesema kuwa watu watatu walimzunguka
mchezaji huyo alipokuwa akielekea katika gari lake na mkewe na mtoto wao wa
mwezi mmoja.
Walimpiga kwa ngumi na mateke kabla ya mmoja ya watu hao kumpiga na jiwe
katika kichwa na kumwacha bila fahamu.
Alifanyiwa upasuaji siku ya jumanne lakini akafariki siku ya jumatano.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Fabian Bordon ameviambia vyombo vya
habari kwamba watu watatu wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo.
Ghasia zinazosababishwa na soka ni tatizo kubwa nchini Argentina.
Kulingana na shirika moja lilisokuwa la kiserikali Salvemos el Futbol,vifo
vinavyosababishwa na ghasia za soka vimeongezeka mwaka huu.
Washukiwa wakuu ni genge la Barras Bravas ambao hudhibiti maneo ya kukalia
katika viwanja vya mpira na barabara karibu na viwanja hivyo.
Chanzo BBC