Hatahivyo ni Manchester United walioona lango la Liverpool kupitia bao la nahodha
wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza.
Yuan Mata alifanya mambo kuwa mbili bila baada ya kufunga krosi iliopigwa na
Young,bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea.

lakini Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya
Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united
iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney.
Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi
huku Kipa wa Manchester akinyaka mashambulizi hayo.
Na baada ya dakika kadhaa Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya
safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.
Chanzo: BBC