Alisema siku hiyo
ya tukio mshtakiwa alikutana na mtoto huyo njiani akielekea nyumbani kwao ndipo
alipomshika mkono na kwenda naye kwenye pagala la nyumba katika mtaa huo.
Mpanda. Kijana mmoja aitwaye Michael Edward (25) mkazi wa
Mtaa wa Mji wa Zamani, Mkoa wa Katavi amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada
ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa
miaka saba.
Hukumu hiyo
iliyovuta hisia za watu wengi mjini Mpanda, ilitolewa juzi na Hakimu mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya Mahakama
kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa pande zote mbili.
Awali, akisoma
maelezo ya upande wa mashtaka Mwendesha Mashtaka, Kulwa Sikwesa alidai
mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 9, 2014, saa 12 jioni
katika eneo la Mji wa Zamani
Alisema siku hiyo
ya tukio mshtakiwa alikutana na mtoto huyo njiani akielekea nyumbani kwao ndipo
alipomshika mkono na kwenda naye kwenye pagala la nyumba katika mtaa huo.
Mwendesha mashtaka
huyo aliieleza Mahakama hiyo kuwa, baada ya kuingia naye ndani mshtakiwa alitoa
kisu na kuchoma kwenye ubao aliokuwa amemshikisha mtoto huyo ikiwa ni ishara ya
kumtishia kisha alimwambia endapo atakataa kulawitiwa au akipiga kelele
atamuua.
Sikwesa alidai
baada ya vitisho hivyo ndipo mshtakiwa alipomvua nguo mtoto huyo na yeye
suruali na kutoa sehemu zake za siri na kuupaka mate na kisha kuanza kumlawiti
mtoto huyo kwa nguvu. Alidai baada ya kumlawiti alimtishia kutotoa siri hiyo
lakini mtoto huyo baada ya kufika kwa wazazi wake alilazimika kuwaambia
kutokana na maumivu aliyokuwa nayo na ndipo walipotoa taarifa Polisi kabla ya
kukamatwa.
Chanzo Mwananchi