Kikosi cha kupambana na majambazi
Watu watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa wamevalia makoti meusi wamevamia kwenye mji mdogo wa Sirari na kufanikiwa kupora shilingi za kitanzania milioni 45 na shilingi Elfu Hamsini za Kenya, kutoka kwenye duka la Dickson Ntali (32).
Katika purukushani hizo watu wawili wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na mmoja miongoni mwa watu hao ni mwalimu wa shule ya msingi Sirari aliyefahamika kwa majina ya Mataigwa Muhono (39) ambaye amepigwa risasi mguuni.
Mtu mwengine aliyejeruhiwa katika uhalifu huo kwa kukatwa mapanga ni mdogo wake mwenye duka la Mpesa, Mara Masabi (23) ambaye ndiye aliyekuwa akitoa huduma.
Kaimu Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime Rolya amesema kuwa majambazi hao walifanikiwa kukimbia baada ya kuona wafanya biashara wengine wameanza kuwazingira wakiwa na siraha.
MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA>>