
Watu wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya jaribio lao la kutaka kupora fedha zaidi ya shilingi milioni 100 katika kiwanda cha kutengeneza chokaa cha Nelkanth kilichopo eneo la Amboni jijini Tanga kushindikana.
Kaimu kamanda
wa polisi mkoani Tanga kamishina msaidizi wa polisi Juma Ndaki amewataja
majambazi waliouawa kuwa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni jijini Dar es
Salaam na mwinyimkuu Hamisi mkazi wa mtaa wa chanika ambao walikuwa wakitumia
usafiri wa pikipiki aina ya boxer huku wenzao wawili wakikimbia kusikojulikana.
Wakielezea
vyema tukio hilo baadhi ya wafanyakazi na walinzi wa kiwanda hicho wamesema
majambazi hao baada ya kuingia ndani ya geti la kiwanda hicho walikwenda moja
kwa moja katika chumba cha mhasibu na walipofika walianza kunyonga mhasibu
lakini wakati wa kujitetea ndipo sekretari wa mhasibu alipotoka nje na kupiga
mayowe kuashiria bosi wake amevamiwa na majambazi. Endelea>>