JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/24
3 Januari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
3 Januari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 593 za kazi kwa ajili ya wakala wa
vipimo kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
-Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-Computer Certificate
-Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira Hairuhusiwi
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika
Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,
Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
1.0WAKALA WA VIPIMO
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Viwanda na
Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245,
mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa
amri ya Serikali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei,
2002. Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda mlaji kwa kuhakiki vipimo vyote
vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira.
Nafasi hizi zitajazwa katika ofisi za Wakala wa Vipimo zilizoko Makao Makuu na katika
Mikoa yote Tanzania Bara.
1.1 AFISA UGAVI MKUU DARAJA LA I - NAFASI 1 (INARUDIWA)
1.1.2 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushauri juu ya Sera ya Ununuzi na Ugavi katika Wakala;
· Kushauri juu ya Mfumo wa Mtandao wa Ununuzi na Ugavi kwa kutumia kompyuta, “e-
procurement”;
· Kutathmini taarifa ya vifaa vinavyotumika na Wakala ili kujua aina ya kasi ya vifaa husika kwa
hatua zaidi;
· Kusimamia utayarishaji wa Mpango wa manunuzi wa Wakala;
· Kusimamia utayarishaji wa makisio ya vifaa vinavyohitajika katika Wakala;
· Kusimamia upimaji wa utendaji wa Maafisa Ugavi walio chini yake;
· Kumshauri Mtendaji Mkuu kuhusu namna bora kutekeleza majukumu yanayohusu ununuzi, utunzaji na ugavi katika Wakala;
1.1.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya Ugavi na Shahada/Stashahada ya Uzamili katika fani za Biashara
au Ugavi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa, na uzoefu wa
kazi usiopungua miaka kumi na mbili (12).
1.1.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 7 kwa mwezi
1.1.5 MCHUMI MKUU DARAJA LA I- NAFASI 1 (INARUDIWA)
1.1.6 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuratibu na kuhuisha upangaji na udhibiti wa mipango ya Wakala;
· Kushiriki katika shughuli za kuandaa mipango, miongozo na nyaraka mbalimbali za Wakala;
· Kuchambua, kudhibiti na kuoanisha Bajeti ya Wakala kwa kushirikiana na Wizara mama;
· Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo;
· Kutoa picha kamili ya uchumi wa Wakala na maendeleo yake kwa vipindi vya muda mfupi na kati;
· Kutayarisha miongozo ya maendeleo ya kila mwaka;
· Kutayarisha na kusimamia mifumo ya shughuli za mipango ya maendeleo;
· Kusimamia mwenendo wa kiuchumi wa Wakala na kutoa ushauri;
· Kusimamia upimaji wa utendaji wa watumishi walio chini yake;
1.1.7 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Uzamili (Masters/Postgraduate Diploma) ambao wamejiimarisha katika mojawapo ya fani zifuatazo Uchumi (Economics), Takwimu (Statistics),
Sayansi ya Uchumi au Kilimo (Bsc. Agriculture Economics & Agri Business) kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
· ujuzi wa kutumia kompyuta na uzoefu wa kazi ya uchambuzi wa masuala ya kiuchumi kwa muda usiopungua miaka kumi na mbili (12).
· Waombaji wenye Shahada ya Falsafa ya (Phd) katika fani husika au watakaokuwa
wamechapisha makala zisizopungua sita (6) zinazohusiana na fani mbalimbali za uchumi
watafikiriwa kwanza.
1.1.8 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 7 kwa mwezi.
2.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 24
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili aweze;
· Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za kupitisha
bomba kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
· Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu wa miradi kufanya kazi yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu wa miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
· Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka
Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi
Daraja III (Water Works Technician Geometric).
2.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
3.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atafanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
· Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
· Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
· Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
· Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
· Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka
Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi
Daraja III (Mitambo Ya Maji (Pampu).
3.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
4.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) – NAFASI 12
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
· Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na
usafi wa mazingira;
· Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa
mazingira;
· Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme vya miradi ya maji
na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
· Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme,
mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa
dharura.
· Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
· Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).
4.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
5.0 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE ENGINEER –
NAFASI 2
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi
yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya
ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
· Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya
miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
· Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu
ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora
unaokusudiwa.
· Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project
proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
· Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
· Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
· Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya
miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
· Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji
kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource
Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
5.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
6.0 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi
yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya
ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
· Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya
miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
· Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu
ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora
unaokusudiwa.
· Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project
proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
· Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
· Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
· Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya
miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
· Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji
kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource with
GIS) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
6.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
7.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 31
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
· Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
· kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
· kulinda Nyara za Serikali
· Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi
· Kusimamia matumizi ya magari ya doria
· Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kutunza
takwimu zao
· Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
· Kudhibiti moto katika hifadhi
· Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
· Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
· Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha
Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
8.0 MHIFADHI MAMBO YA KALE II (CONSERVATORS OF ANTIQUITIES GRADE II) –NAFASI 4
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushiriki katika kutunza na kuhifadhi mazingira ya vituo na maeneo ya Mambo ya
Kale.
· Kushiriki katika kufanya kazi za ukarabati wa majengo
· Kushiriki katika kuboresha maeneo yenye umuhimu ya kihistoria.
· Kushiriki katika kufanya kazi za ufundi
· Kuratibu na kupokea wageni mbalimbali wanaotembelea Vituo vya Mambo ya
Kale.
· Kushiriki katika kufanya utafiti na uhifadhi.
· Kushiriki kuandaa tathmini ya maeneo ambayo yamefanyiwa utafiti na uhifadhi.
· Kuratibu ushauri wa kurekebisha vipengele vya Sheria ya Mambo ya Kale.
· Kuendesha mafunzo ya Elimu ya Jamii kuhusu masuala ya utafiti na uhifadhi kwa
njia ya semina, warsha na vipindi vya radio.
· Kushiriki katika kuandaa vipindi vya TV na Radio
· Kushiriki katika kuandaa kazi za maabara.
· Kushiriki katika kuandaa kumbukumbu za mambo ya kale.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada ya juu ya Sayansi ya Jamii au Sayansi ya
Asili, waliojiimarisha (major) katika mojawapo ya michepuo ya Jiologia, elimu ya
viumbe, Akiolojia, Anthropolojia, Jiografia, Historia, Paleontolojia au Ethnolojia
kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
9.0 AFISA ELIMU DARAJA LA II (EDUCATION OFFICER GRADE II) – KISWAHILI(NAFASI 16)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na
Watoto.Walimu hawa watafanya kazi ya kufundisha katika vyuo vya maendeleo ya
wananchi vilivyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufundisha somo la Kiswahili katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
· Kuandaa maazimio ya kazi, maandalio ya masomo, zana za kufundishia
/kujifunzia, mazoezi ya wanafunzi na majaribio.
· Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa lengo la kutathmini maendeleo
ya wanachuo.
· Kuandaa mazoezi ya kazi kwa wanachuo na kusahihisha.
· Kuandaa taarifa za kitaaluma na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya
wanachuo na kuwasilisha katika mamlaka husika.
· Kufanya tafiti mbalimbali za kielimu.
· Kushika zamu na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo.
· Kutunza na kudhibiti matumizi ya vifaa katika sehemu aliyokabidhiwa.
· Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi za juu kuhusu masuala mbalimbali
kulingana na majukumu aliyopewa.
· Kutoa ushauri nasaha na kuwalea wanachuo kwa kuwaandaa kiakili,kimwili,kitabia na kimwenendo ili waweze kujua wajibu wao kwa jamii
· Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Chuo.
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali waliosoma somo la Kiswahili. Aidha kipaumbele ni walimu wenye
Shahada ya Elimu ya Watu Wazima katika somo tajwa hapo juu.
· Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGTS D kwa mwezi.
10.0 AFISA ELIMU DARAJA LA II (EDUCATION OFFICER GRADE II) – KIINGEREZA (NAFASI 14)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na
Watoto.Walimu hawa watafanya kazi ya kufundisha katika vyuo vya maendeleo ya
wananchi vilivyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
10.1MAJUKUMU YA KAZI
· Kufundisha somo la Kiingereza katika vyuo vya Maendeleo ya wananchi.
· Kuandaa maazimio ya kazi, maandalio ya masomo, zana za kufundishia
/kujifunzia, mazoezi ya wanafunzi na majaribio.
· Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa lengo la kutathmini maendeleo
ya wanachuo.
· Kuandaa mazoezi ya kazi kwa wanachuo na kusahihisha.
· Kuandaa taarifa za kitaaluma na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya
wanachuo na kuwasilisha katika mamlaka husika.
· Kufanya tafiti mbalimbali za kielimu.
· Kushika zamu na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo.
· Kutunza na kudhibiti matumizi ya vifaa katika sehemu aliyokabidhiwa.
· Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi za juu kuhusu masuala mbalimbali
kulingana na majukumu aliyopewa.
· Kutoa ushauri nasaha na kuwalea wanachuo kwa kuwaandaa kiakili,kimwili,kitabia na kimwenendo ili waweze kujua wajibu wao kwa jamii
· Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Chuo.
10.2SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali waliosoma somo la Kiingereza.Aidha kipaumbele ni walimu wenye
shahada ya Elimu ya Watu Wazima katika somo tajwa hapo juu.
· Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
10.3MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGTS D kwa mwezi.