
Wilson alisema kabla ya kujinyonga, alimpiga mtoto wake wa miaka minane na
kumjeruhi vibaya kichwani na kuhisi kuwa amemuua.
Muleba. Mkazi mmoja wa Kijiji cha Bushembe, wilayani
Muleba, mkoani Kagera amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kumpiga mwanaye
na kumpasua kichwa.
Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Dickson Wilson alimtaja mtu huyo kuwa ni
Godfrey Joseph, mkazi wa Kijiji cha Bushembe na kwamba tukio hilo lilitokea
Januari 3, mwaka huu.
Wilson alisema kabla ya kujinyonga, alimpiga mtoto wake wa miaka minane na
kumjeruhi vibaya kichwani na kuhisi kuwa amemuua. Alisema hilo ni tukio la pili
kwa marehemu kulifanya la kujeruhi watu wa familia yake, kwani awali alimpiga
mkewe na kumchoma na spoku ya baiskeli iliyokuwa na moto sehemu zake za siri,
kitendo kilichomfanya mwanamke huyo aondoke nyumbani.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rubya alikolazwa mtoto huyo kwa matibabu,
Modesti Rwakahebula alisema wanaendelea kumtibu na hali yake bado
haijatengamaa.
Chanzo Mwananchi