Ulevi wa kupindukia unasemekana kuwa ndio chanzo kikuu cha tukio hili la mauaji.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Faustine Macha (45) ameuawa kwa kupigwa na rungu kichwani na
kuvunjwa miguu kisha kutupwa shambani.
Kamanda
Moita alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni katika Kijiji cha
Kinango wilayani Moshi Vijijini. Alisema marehemu alipigwa na watu wawili baada
kulewa na kuanza kutukanana.
Kamanda
Moita alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji. Mwili wa
marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Kilema.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi