Alisema
kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa na pikipiki, alimchukua na kumpeleka kwenye
vichaka ambavyo viko jirani na barabara huku mwenzake akiwa analia kuomba
msaada.
Dereva bodaboda Ismail Lucas (16), mkazi wa
Kwa Mathias wilayani Kibaha mkoani Pwani, anatuhumiwa kumlawiti mtoto ambaye ni mwanafunzi wa Chekechea.
Mama
wa mtoto huyo (jina limehifadhiwa) alisema kuwa kutokana na tukio hilo, mwanawe
(jina limehifadhiwa) alijeruhiwa vibaya.
Alisema
kuwa tukio hilo lilitokea saa 3:00 asubuhi eneo la Tanita wakati mtoto huyo
alipokuwa akitokea dukani akiwa ameongozana na mwenzake, mtoto wa mama yake
mkubwa mwenye umri wa miaka saba, ambaye alikuwa amewaagiza mkate.
“Mama
yake mkubwa aliwatuma dukani Kwa Mrisho ambapo walinunua mkate na walipokuwa
wakirudi, walikutana na mtuhumiwa ambaye alimrubuni mwanangu kuwa ameangusha
chenji iliyorudi dukani hivyo aende
akampe,” alisema.
Alisema
kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa na pikipiki, alimchukua na kumpeleka kwenye
vichaka ambavyo viko jirani na barabara huku mwenzake akiwa analia kuomba
msaada.
“Alikwenda
naye huko vichakani na kumfanyia vitendo hivyo,
mama mmoja Clara Edwin alikuwa akipita hapo na alipomwona mtoto aliyekuwa
akilia alimwuliza imekuwaje, akamwambia
mwenzangu kachukuliwa na mtu asiyemfahamu na kuelekea eneo la tukio, ndipo
mtuhumiwa alipokimbia na kuacha pikipiki yake,” alisema.
Alisema
kuwa yeye hakuwepo nyumbani, lakini alijulishwa kuwa mwanawe kafanyiwa mchezo
huo, ambapo alipomwona mwanawe akiwa kwenye hali ile, alipoteza fahamu.
“Majirani
walinisaidia baada ya muda nilizinduka na kumpeleka mtoto kituo cha Polisi cha
Kwa Mathias na baadaye Hospitali ya Mkoa ya Tumbi kwa ajili ya matibabu ambapo
hadi sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu,” alisema.
Kwa
upande wake, Clara ambaye ndiye aliyemuokoa mtoto huyo, alisema yeye baada ya
kwenda kule vichakani mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana na wasamaria waliipeleka pikipiki hiyo kwenye kijiwe
anachofanyia kazi na ndipo walipobaini kuwa ni ya Lucas.
“Wasamaria
wema wakishirikiana na madereva bodaboda wenzake, walifika nyumbani kwao na
kumkuta mlezi wake ambapo walimwambia asimruhusu kuondoka hadi polisi
watakapofika, ambapo walimchukua na kumpeleka kituoni,” alisema.
Akithibitisha
kutokea tukio hilo, Kamanda wa Polisi
mkoani Pwani, Ulrich Matei (pichani juu) alisema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na
atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika