Sasa wapiganaji hao wamebuni
halmashauri ya usalama kuongoza nchi hadi bunge la muda litakapoundwa.
Bomu limelipuka nje ya ikulu
ya rais wa Yemen, katika mji mkuu, Sanaa, mji ambao sasa unadhibitiwa na
wapiganaji wa madhehubu ya Shia, wa Houthi
Inaarifiwa kuwa waasi wawili
wa Houthi walijeruhiwa.
Hapo jana wapiganaji hao
walilivunja bunge kabla ya kudhibiti madaraka.
Wapiganaji wa Hauthi
Sasa wapiganaji hao wamebuni
halmashauri ya usalama kuongoza nchi hadi bunge la muda litakapoundwa.
Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa limesema kuwa liko tayari kuchukua hatua zaidi, iwapo wapiganaji hao
hawatarudi haraka kwenye mazungumzo, kuhusu kipindi cha mpito cha kuelekea
kwenye demokrasi.
Baraza jiiya limewataka
wapiganaji wamuachilie huru rais wa Yemen, waziri mkuu, na baraza la mawaziri
kutoka kifungo cha nyumbani.
Chanzo: BBC