Mbunge mmoja ameuawa kwa kupigwa risisi, Walinzi wake wawili,dereva pia nao wameuawa.
Mbunge mmoja ameuawa kwa kupigwa risisi kwenye mji mkuu
wa kenya Nairobi.
Ripoti za polisi zinasema kuwa mbunge huyo wa Kabete,
eneo lililo nje kidogo ya mji wa Nairobi aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa
kuamkia leo.
Walinzi wake wawili,dereva pia nao wameuawa.
Polisi wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha walilifuata
gari la mbunge huyo kutoka eneo la Westlands kabla ya kulimiminia rasasi ndani
ya mji wa Nairobi.