Miili ya watu 8 tu kati ya 50 waliokufa kwa ajali ya juzi,
iliyohusisha basi la kampuni ya Majinja yenye namba za usajili T438 CED na Lori
lenye namba za usajili T 689 APJ, katika eneo la Changarawe, Mafinga Mkoani
Iringa, ndiyo iliyotambuliwa mpaka kufikia jana mchana.
Idadi ya Marehemu hao iliongezeka kutoka 42 waliokufa mapema
juzi hadi 50. Mmoja wa hao walio ongezeka aliyekuwa amelazwa katika hospitali
ya mkoa wa Iringa, ametambuliwa kwa majina ya Oswad Mwinuka (58)
Mganga Mkuu wa mkoa wa Iringa, Robert Salim alisema kati ya
maiti 27 waliofikishwa hapo kutoka Mafinga ni wanane tu waliotambuliwa na ndugu
zao, wengi wao kutoka jijini Mbeya.