Taarifa za awali kutoka vyanzo mbalimbali juu ya Ajali iliyotokea juzi kwa kuhusisha basi la kampuni ya Majinja yenye namba za usajili T438 CED na Lori
lenye namba za usajili T 689 APJ, katika eneo la Changarawe, Mafinga Mkoani
Iringa. Vilidai kuwa abiria wengi waliokufa katika ajali hiyo walikuwa ni wanafunzi wa chuo kikuu
cha Dar es salaam.
Lakini kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi
ameeleza kuwa miili ya abiria wengi ambayo inaendelea kutambuliwa walikuwa ni
wafanya biashara wa eneo la Soweto, mjini Mbeya.
Kamanda Mungi alisema kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa barabara katika eneo la ajali na mwendo kasi.
Baada ya magari hayo kugongana, Kontena lililokuwa limepakiwa katika lori hilo
lilifyatuka na kudondokea basi hilo, hali iliyosababisha mauti na majeruhi
wengi katika ajali hiyo.