Stamili
Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero,  mkoani Morogoro
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma mwanae na kumjeruhi mikono kwa
madai ya kuiba ugali.
 Mikono ya Mtoto anayedaiwa Kuchomwa
Mama huyo alimuunguza mwanaye
 Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji
 mbalimbali wa kata ya Mng’eta.
Wakizungumzia tukio hilo Jerome
Chulu na Jeneth Hetela,  walisema unyanyasaji huo  ulishuhudiwa na
majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua
mtoto huyo kumpeleka of isi  ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye
hospitali.
Walibainisha baadaye kuwa polisi
 walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye
 inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo
aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine nyumbani.
 Polisi  walithibitisha
tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa
huyo.Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu
wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
 Chanzo Nipashe
