Serikali katika wilaya ya Mtwara imelazimika kumuhamisha kituo cha kazi Daktari aliefahamika kwa jina la Isabella Tilia ili kumnusuru kupigwa na wananchi wa kata ya Mkunwa Wilaya ya Mtwara vijijini wanaomtuhumu kutumia lugha chafu kwa wagonjwa sambamba na kushindwa kutoa huduma baada ya saa za kazi.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma Ally amelazimika kufanya maamuzi hayo baada ya kuzuka mgogoro mzito baina ya wananchi wa kata ya Mkunwa na daktari huyo  maamuzi ambayo ameyatoa katika mkutano baina yake na wafanyakazi wa zahanati ya Mkunwa,viongozi wa vijiji na wazee maarufu wa kata hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara vijijini Dokta Juma Gumbo amekiri kupata malalamiko ya wananchi dhidi ya Dokta Isabella,huku baadhi ya watendaji wa zahanati hiyo wakilalamikia kuendelea kutishiwa maisha na wananchi.
 
Top