Picha: Sehemu Za Binadamu zilizoathirika na Magonjwa ya Ngono
NINI KIJANA ANAPASWA KUJUA KUHUSU MAGONJWA YA NGONO?
Magonjwa
ya Ngono ni magonjwa yanayoambukizwa kwa tendo la kujamiiana na mtu
aliyeambukizwa magonjwa hayo bila kutumia Kondomu. Magonjwa haya huweza
kuwapata watu wa rika zote hususani wale walio katika umri wa kuzaa
(Kati ya miaka 15 - 49)
Vijana
walio katika umri kati ya miaka 10 hadi 24 wanawakilisha 1/3 ya idadi
ya wakazi wote wa Tanzania. Kundi hili liko katika hatari zaidi ya
maambukizi ya magonjwa ya Ngono kwakuwa wanapobalehe wanapata hisia za
kupenda na pia hamu ya kufanya tendo la kujamiiana kujitokeza kwa nguvu
Hali
hii huchochewa na Vichocheo/Homoni vilivyomo mwilini ambavyo katika
kupanda katika kupanda na kushuka husababisha hisia za kufanya tendo la
Kujamiiana.
Hivyo
basi ikiwa watakosa Ufahamu wa Kutosha Kuhusu miili yao wanaweza
kujiingiza katika tabia Hatarishi za Kujamiiana bila Kondomu na mwenzi
zaidi ya Mmoja.
Read More>>
Read More>>