Mji wa Alagarno ambao uko katika jimbo la Borno, uko karibu
na mji wa Chibok ambako wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara na kundi la
wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wiki tano zilizopita.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni kufanywa nchini Nigeria
wakati nchi hiyo ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta zaidi ya wasichana
miambili waliotekwa nyara na Boko Haram.
Juhudi hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa
kimataifa kutoka Israel, Marekani na Uingereza.
Pia limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea
mjini Jos katika jimbo la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne
usiku.
Juhudi za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi
lililofanyika mjini Jos, lilisababishwa na Boko Haram na kwamba huenda ni
ujumbe kwa serikali kuwa wapiganaji hao wanaweza kushambulia wakati wowote
wanapotaka.