Mkazi wa Mkokozi
Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Sara Zefhania mzazi wa Happness Rioba
ambaye alidaiwa kuzamia kwenye ndege jijini Dar es
Salaam na kwenda Zanziba.
Sakata lililokuwa limejitokeza
la mtoto aliyezamia ndege kutokea Jijini Dar es salaam hadi Zanziba
aliyejitambulisha kwa jina la Karine godfrey limeibua sura mpya baada ya
kujikeza kwa mwanamke mmoja mkazi wa Mkuranga wilayani pwani na kudai kuwa mtoto huyo niwakwake.
Mwanamke huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Sarah Zefania, ameeleza kuwa mtoto huyo ni
wakwake na anaitwa Happynes Rioba na si Karine Godfrey kama alivyojitambulisha mwenyewe.
Zefania alisema kuwa sio
kweli kwamba mtoto huyo alikuwa amezamia ndege kama ambavyo alitangazwa na
kituo cha Televisheni, bali ni tabia yake ya kupotea katika mazingira ya
kutatanisha ambayo hutokea mara kwa mara.
Mwanamke huyo aliongeza kuwa
Hakuna ukweli wowote wa mtoto huyo kusindikizwa na dada yake Airport kupanda ndege bali ni
ile tabia yake aliyokuwa nayo ndiyo aliyoitumia.
Alisema kuwa mtoto wake huyo
amekuwa na tabia hiyo tangu zamani, na alishawahi kutoweka kwa kupindi cha
mwezi mzima. Baada ya mama huyo pamoja na ndugu kuhangaika walifanikiwa kumpata
mkoani Mwanza akiwa katika mazingira ya kutatanisha.
Taarifa zilizotufikia leo hii ni kwamba mtoto huyo ametoweka katika nyumba Salama huko Zanziba ambako alikuwa akihifadhiwa Soma zaidi Hapa>>
Taarifa zilizotufikia leo hii ni kwamba mtoto huyo ametoweka katika nyumba Salama huko Zanziba ambako alikuwa akihifadhiwa Soma zaidi Hapa>>