Mheshimiwa Sata
Alikuwa London kimatibabu huku wananchi wadai kutokuwa na taarifa za maendeleo yake hadi kufikiwa na mauti hayo.
HABARI KAMILI
Raisi wa Zambia Mh Michael Sata (77) amefariki
dunia akiwa London ambako alikwenda kwaajili ya matibabu.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hii vimeeleza
kuwa mheshimiwa Sata amefariki jana Jumanne jioni katika hospitali ya King
Edward II huko London. Hata hivyo hospitali hiyo imegoma kuzungumzia chochote
juu ya taarifa hizo.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali ya Zambia
ni kwamba Sata (77) aliondoka nchini Zambia na kwenda London kwaajili ya
matibabu mnamo tarehe 19 mwezi wa Oktoba akitangulizana na familia yake. Serikali
haikuzungumza tena jambo lolote zaidi ya kauli hiyo.
Baada ya taafira hizo, hakukuwepo na taarifa
nyingine tena zilizozungumzia maendelea ya mgonjwa, na badala yake Makamu wa
Raisi Mheshimiwa Wdgar Lungu aliongoza sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru
uliopatikana kutoka kwa Mbritish.
Hadi sasa serikali ya Zambia bado
haikuzungumza chochote kuhusiana na Kifo cha Mheshimiwa Sata ambaye amekuwa
raisi wa Zambia tangu Septemba, mwaka 2011