Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya wa Kihenya
Ndugu wawili wakazi wa Mtaa wa Madafu Tandika jijini Dar es salaam, wamekutwa wamekufa baada ya kunyongwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii, ndugu hao wamefahamika kwa majina ya Makamu Mariamu Buruhani (39), na Nuru Tumwanga (42).

Chanzo cha kubainika kwa tukio hilo la kusikitisha ni baada Makamu ambaye ni mmiliki wa saluni mtaani hapo kuchelewa kufika saluni hapo. hali hiyo ilimfanya mfanyakazi wake mmoja kutuma mtu kwenda kumuangalia nyumbani kwake. 

Baada ya mtu huyo aliyetumwa kufika nyumbani hapo, alikuta mlango upo wazi na alipoingia aliukuta mwili wa Nuru ukiwa Kitandani na mwili wa makamu ukiwa sakafuni sebuleni, Hivyo alikwnda kumuita mwenyekiti wa serikali za mtaa, Madadi Mtwanga na baadae kutoa taarifa polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Temeke, kihenya wa Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa miili ya marehemu hao imefikishwa katika Hospitali ya Temeke ambako uchunguzi wa awali umebaini kuwa ndugu hao wamenyongwa kutokana na kuwa na majeraha shingoni.
Chanzo Mwananchi

FUNGUA MATUKIO MENGINE HAPA>>

 
Top