Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakirusha mabomu ya machozi

Vurugu kubwa imezuka jana katika eneo la makao makuu ya polisi Jijini Dar es salaam kati ya polisi na waandishi wa habari. 


Kasheshe hilo limetokea jana asubuhi katika eneo la makao makuu ya polisi baada ya menyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe kuitwa kutoa maelezo kufuatia taarifa alizozitoa siku chache kushinikiza wananchi wafanye maandamano kupinga kuendelea kwa bunge la katiba.

Kabla ya askari waliokuwa na silaha kukabiliana na waandishi wa habari, walianza na wanachama wa chama cha Chadema ambao walikuwa wakileta vurugu katika eneo hilo kushinikiza baadhi ya wabunge wa Chama hicho kuingia na kusikiliza kile alichokuwa ameitiwa mwenyekiti wao.

Wabunge hao ambao walikuwa wamezuiliwa na jeshi la polisi kuingia katika jengo hilo la makao makuu ya jeshi la Polisi ambamo walimuingiza mwenye kiti wa chama hicho cha Chadema, Freeman Mbowe, walikuwa ni Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iramba Mashariki Tundu Lissu, Mbunge wa Ubungo John Mnyika na mwenzake wa jimbo la Ilemela Ezekiah Wenje.

Baadae mshike mshik huo uliokuwa ukiwakabili wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, ulihamia kwa waandishi wa Habari, ambapo askari walikuwa wakiwazuia kufika katika jengo hilo na kuchukua habari jambo ambalo ni kinyume na haki za waandishi wa habari.

Katika purukushani hizo, waandishi waliumia katika sehemu mbalimbali za miili yao kama vile machoni na sehemu nyingine za viungo vya mwili.


“Waandishi wameumzwa katika sehemu mbalimbali za miili yao walipokuwa wakifanya jitihada za kutekeleza wajibu wao” alisema mtoa habari wetu.
  
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) wakimzuia mwandishi wa habari

 
Mwandishi wa habari akilia kwa machungu maada ya kuumizwa na kikosi cha mbwa wa poilisi
 
Top